Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Saratani ya Damu ( Leukemia)

Utangulizi Saratani ya damu, inayojulikana kitaalamu kama leukemia, ni ugonjwa unaoathiri mfumo wa utengenezaji wa damu mwilini — hasa kwenye mifupa inaozalisha chembechembe za damu (bone marrow). Katika hali ya kawaida, mifupa huzalisha chembe nyekundu za damu, chembe nyeupe (zinazopambana na maambukizi), na chembe sahani (platelets) vinavyosaidia kugandisha damu wakati mtu anapopata majeraha. Kwa wagonjwa wa leukemia, mfumo huu unaharibika na kuanza kuzalisha kwa wingi chembechembe nyeupe zisizo kamili na zisizokomaa, zinazozuia utengenezaji wa chembe zenye afya. Hii husababisha upungufu wa damu, maambukizi ya mara kwa mara, na kushindwa kugandisha damu. Aina Kuu za Leukemia Leukemia hugawanyika katika makundi makuu manne kulingana na kasi ya maendeleo ya ugonjwa na aina ya chembe inayoathirika: Acute Lymphoblastic Leukemia (ALL) Hii ni aina inayosambaa haraka na hutokea zaidi kwa watoto wadogo (miaka 2 hadi 10), ingawa watu wazima pia wanaweza kuathirika. Ni saratani namba moj...
Machapisho ya hivi karibuni

Mawe ya Figo (Kidney Stones)

Utangulizi Mawe ya figo ni moja ya matatizo ya kawaida yanayoathiri mfumo wa mkojo. Mawe haya huundwa kutokana na madini na chumvi zinazokusanyika kwenye figo na kuunda uvimbe mgumu kama jiwe. Mawe ya figo yanaweza kuwa madogo kama mchanga au makubwa kiasi cha kuziba njia ya mkojo. Ugonjwa huu unaweza kusababisha maumivu makali sana, hasa mawe yanapohamia kutoka kwenye figo hadi kwenye kibofu au njia ya mkojo (ureter). Aina za Mawe ya Figo Kuna aina nne kuu za mawe ya figo, ambayo hutegemea muundo wa kemikali: Mawe ya calcium oxalate: Haya ndiyo aina ya kawaida zaidi ya mawe ya figo. Hupatikana wakati kuna kiwango kikubwa cha kalsiamu na oxalate kwenye mkojo. Mawe ya uric acid: Haya hutokea wakati mkojo unakuwa na kiwango kikubwa cha asidi. Mara nyingi yanaathiri watu wanaokula vyakula vyenye kiwango kikubwa cha  nyama nyekundu au wale wenye historia ya ugonjwa wa jongo (gout). Mawe ya struvite: Mawe haya yanaonekana zaidi kwa wanawake na hutokea baada ya maambukizi ya njia ya m...

Maambukizi ya Sikio la Kati (Otitis Media)

  Utangulizi Maambukizi ya Sikio la Kati(Otitis media) ni ugonjwa wa maambukizi yanayoathiri sikio la kati. Sikio la kati ni eneo lililo nyuma ya ngoma ya sikio, ambalo lina nafasi ndogo yenye hewa inayohusiana na sauti. Watoto ndiyo waathirika wakuu wa ugonjwa huu, ingawa watu wazima pia wanaweza kuugua. Maambukizi ya Sikio la Kati inaweza kusababishwa na virusi au bakteria, na mara nyingi huja baada ya kuambukizwa kwa mfumo wa hewa kama mafua au homa. Aina za Maambukizi ya Sikio la Kati Kuna aina kuu tatu za Maambukizi ya Sikio la Kati: Maambukizi ya Sikio la Kati mapya (Acute Otitis Media - AOM) : Hii ni maambukizi ya ghafla kwenye sikio la kati yanayosababisha maumivu makali na dalili kama homa. AOM ni matokeo ya virusi au bakteria, ambapo kioevu hukusanyika kwenye sikio la kati. Maambukizi ya Sikio la Kati yenye usaha (Otitis Media with Effusion - OME) : Hali hii hutokea baada ya AOM ambapo kioevu (liquid)  kinabaki kwenye sikio la kati bila dalili za maambukizi makali. I...

Ugonjwa wa Fistula ( Rectovaginal Fistula)

  Fistula ni nini? Fistula ni tundu lisilo la kawaida linalounganisha sehemu mbili za mwili ambazo kwa kawaida hazipaswi kuungana. Kwa wanawake, hali hii mara nyingi hutokea kati ya  sehemu za siri za mwanamke  na kibofu cha mkojo au njia ya haja kubwa , hivyo kumfanya mgonjwa kushindwa kuzuia haja au kutokwa na haja k ubwa katika  njia ya uzazi .  Mara nyingi husababishwa na kujeruhiwa kwa sehemu hizo wakati wa kujifungua hasa kwa wanawake wanaozaa katika umri mdogo au wanaokosa msaada stahiki wakati wa kuzaa. Kwa mujibu wa shirika la afya duniani,  inakadiriwa kuwa wanawake zaidi ya milioni mbili kutoka Afrika na Asia wanaishi na ugonjwa huu, bila kupatiwa matibabu yoyote, kwa upande wa Tanzania wengi wamekua wakitafuta msaada kwa waganga wa jadi.   Nini Husababisha Fistula? Ugonjwa wa Fistula unaweza kusababishwa na mambo kadhaa ikiwemo yafuatayo; Majeraha wakati wa kujifungua, Maambukizi ya Mfumo wa uzazi (PID), Mgonjwa ya utumbo mpana kama vile Cr...

Kukua Kwa Tezi Dume ( Benign Prostatic Hyperplasia- BPH)

Kukua Kwa Tezi Dume ( Benign Prostatic Hyperplasia) ni nini? Ni ukuaji wa tezi dume ambalo lipo kwenye mfumo wa uzazi wa mwanaume hivyo kusababisha matatizo mengi hasa ya kibofu, figo na  njia ya mkojo kwa ujumla. Hii hutokana na kuzibwa kwa njia ya mkojo kitu ambacho huleta madhara kwenye viungo husika. Tatizo hili huzidi  kadri umri  unavyoongezeka. Kwa kawaida ukubwa wa tezi ni sawa na kipira cha golf , lakini linaweza kukua hadi kufikia ukubwa wa chungwa hivyo kusababisha matatizo. Tezi dume kazi yake ni kutoa majimaji ya shahawa ( semen ) yanayosaidia kulinda, kurutubisha na kusafirisha mbegu za kiume  ( sperms ) ndani ya mfumo wa uzazi wa mwanamke. Karibu nusu ya wanaume wenye umri kati ya miaka 51 mpaka 60 na zaidi ya asilimia 90 ya wenye umri wa miaka 80 na zaidi wana tatizo hili. Ukuaji wa tezi dume sio saratani lakini wakati mwingine vyote viwili  humpata mtu mmoja. Dalili Kujisikia kukojoa muda wote au kushindwa kubana mjoko, Kukojoa kila mara ha...

Homa ya Mfumo wa Uzazi (Pelvic Inflamatory Disease- PID )

Homa ya Mfuko wa Uzazi ni nini? Ni magonjwa yanayompata mwanamke katika uke, shingo ya uzazi,mfuko wa uzazi, mirija ya uzazi na sehemu inayozunguka mfumo wa uzazi. Karibu asilimia 85 ya watu wanaopata homa hii hutokana na magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana, wengi wao wakiwa na vimelea vya bakteria kama vile  kisonono (gonorrhoea) , kaswende (syphilis) , klamidya n.k. Wakati mwingine mgonjwa hupata homa hii kutokana na bakteria ambao kawaida huwa wapo mwilini na hawana madhara lakini kwa sababu mbalimbali kama kupungua kwa kinga, kisukari, saratani, upasuaji, kuwa na magonjwa ya mfumo wa chakula n.k wanasababisha homa.   Dalili Maumivu makali chini ya kitovu na kiunoni, Maumivu wakati wa tendo la ndoa, Maumivu wakati wa kukojoa, Maumivu makali au kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi, Kutokwa na majimaji yenye harufu kali  na rangi ya njano, kijani au kahawia ukeni, Kuwa na homa jotoridi 38.3 au zaidi, Kujisikia uchovu, kichefuchefu n.k.   Sababu Homa ya...

Saratani ya Matiti (Breast Cancer)

Utangulizi Saratani ya Matiti ni nini? Ni aina ya saratani inayoathiri matiti au maziwa kwa mwanamke au nadra pia kwa mwanaume. Hii hutokana na chembehai( cells) za sehemu yoyote ya ziwa au yote mawili kukua kuliko kawaida na kusababisha uvimbe, maumivu, kutokwa na majimaji,damu au usaha kwenye matiti. Wakati mwingine aina hii ya saratani inaweza kusambaa sehemu nyingine za mwili kama vile kwenye kwapa, misuli ya kifua, mishipa ya damu, shingoni n.k.  Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), mwaka 2020, wanawake milioni 2.3 waligunduliwa kuwa na saratani ya matiti, takriban laki saba walifariki kwa saratani ya matiti. Kutoka mwaka 2015 hadi 2020 wanawake milioni 7.8 waligunduliwa kuwa na maradhi hayo, kuifanya saratani ya matiti kuwa ya kwanza kwa kuenea duniani. Ni muhimu kutambua kwamba sio kila uvimbe uliopo kwenye maziwa ni saratani, hivyo ni vyema kumuona Daktari unapokuwa na dalili yoyote nitakayotaja hapo chini kwa ajili ya uchunguzi zaidi.  Nini husababisha sarata...