Utangulizi Unapokula chakula cha wanga kama vile ugali,wali, matoke,mihogo,viazi n.k hubadilishwa kuwa sukari iitwayo glukozi. Glukozi ni miongoni mwa vyanzo vikuu vya nishati.Sukari hii hudhibitiwa na homoni iitwayo insulini,inayotolewa na kiungo kinachoitwa kongosho kilichopo katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Kisukari ni ugonjwa unaosababisha na mwili kushindwa kubadili glukozi kuwa nishati,hivyo kusababisha kiwango cha sukari kuwa kingi katika mzunguko wa damu. Kwa lugha ya kitaalamu huitwa Diabetes Mellitus .Kuna aina nyingi za kisukari lakini kwa kurahisisha,kwa leo tutagawanya katika aina kuu tatu. Aina ya kwanza Pia huitwa inslini tegemezi. Kongosho hushambuliwa na magonjwa ya kingamaradhi(autoimmune) na kushindwa kutoa homoni ya insulini. Kisukari cha aina hii humpata mtu akiwa katika umri mdogo. Dawa yake ni mgonjwa kupatiwa insulini. Aina ya pili Huu ni ugonjwa wa kurithi. Aina hii huwapata zaidi watu wanene na wanene kupindukia. Watu wanene ...
Elimu ya Afya Kiganjani Mwako