Utangulizi Unaweza kuwa na shinikizo la damu (presha) kwa muda mrefu bila kuwa na dalili zozote. Muda wote huu ingawa unakuwa hauna dalili, uwepo wa shinikizo la damu huendelea kuathiri mishipa ya damu na kusababisha madhara makubwa mwilini kama vile magonjwa ya moyo na kiharusi. Hivyo ni vizuri kujipima mara kwa mara ili kuepuka kuchelewa. Shinikizo la damu hutokea taratibu kwa kadri umri unavyozidi kuongezeka, hivyo kuathiri karibu kila mtu anapofikia umri mkubwa. Upimaji wake ni rahisi kwa hiyo ni vema ukapima ili kuweza kupambana na ugonjwa huu kwa msaada wa daktari. Dalili Watu wengi wana shinikizo la damu bila kujua au kuwa na dalili. Ni wachahe wanaweza kuwa na dalili kama vile kuumwa kichwa,kutokwa na damu puani na kupata shida ya kupumua. Dalili hizi si maalumu ( spesific) na mara nyingi hazitokei mpaka shinikizo linapokuwa katika kiwango kinachohatarisha maisha. Shinikizo la damu hutokea kwa namna mbili; Kwanza: Hutokea bila u...
Elimu ya Afya Kiganjani Mwako