Virusi vya Korona ni nini?
Virusi vya Corona (Cov) ni familia ya
virusi vinavoysababisha ugonjwa kuanzia mafua ya
kawaida hadi magonjwa makali zaidi
kama vile matatizo ya kupumua (MERS-CoV) na SARS-CoV.
Mwishoni mwa Mwaka 2019,huko nchini
China katika mji wa Wuhan kulitokea mlipuko wa
virusi vya korona vilivyopewa jina la COVID-19(
Corona virus disease 2019)
Baada ya muda mfupi mlipuko huo
ulienea sehemu mbalimbali Duniani,hasa katika nchi za
Korea ya Kusini, Italya, Iran na Nchi
mbalimbali za Ulaya.
Kulingana na maambukizo kusambaa
haraka, Shirika la Afya duniani lilitangaza mlipuko
huu kuwa wa ngazi ya Pandemia tarehe 30 Januari 2020.
Hadi sasa ugonjwa huu umeenea kote
Duniani na kusababisha maambukizi kwa zaidi ya watu 2,320,000 vifo zaidi ya watu 160,000; huku nchi ya Marekani ikiwa
inaongoza kwa idadi ya wagonjwa wanaozidi laki saba.
Ugonjwa wa korona unaambukizwaje?
Ugonjwa wa korona unaambukizwa kwa
virusi vinavyoachwa hewani kwa kupiga chafya au kukohoa na kwa njia ya mgusano baina ya watu
pale panapokuwa na mgonjwa.
Ukimgusa mtu halafu ukagusa
macho,pua, mdomo au kula chakula bila kunawa mikono.
Kumbuka sio kila mtu mwenye korona
anakuwa na dalili,hivyo hasa watu wasio na dalili
ndio wana uwezekano mkubwa wa
kusambaza virusi.
Dalili.
Dalili zake ni pamoja na;
- Homa,
- Kikohozi kikavu,
- Shida katika kupumua,
na katika hali ngumu zaidi,
maambukizi yanaweza kusababisha;
Homa ya mapafu (pneumonia),Kukosa
pumzi, Kushindwa kufanya kazi kwa figo na hata kifo.
Jinsi ya Kujikinga.
- Epuka mkusanyiko wa watu kadri inawezekana, na kama itakulazimu kuwa kwenyemkusanyiko jaribu kuwa katika umbali wa mita 1 au zaidi kati ya mtu na mtu,
- Nawa mikono kwa sabuni (kwa sekunde 20 au zaidi) mara kwa mara hasa unapokisha vitu au watu,
- Epuka kugusa uso mara kwa mara,
- Acha kuvuta sigara,
- Tumia vifaa vya kujikinga unapokuwa kwenye mkusanyiko wa watu kama vile maski na gloves.Haishauriwi kutumia vifaa hivi kama upo peke yako,
- Kaa nyumbani na kujitenga unapohisi dalili hizo hapo juu.
- Nenda hospitali kama daili zinazidi.
Kinga na tiba;
Mpaka sasa hakuna kinga,chanjo wala
tiba ya virusi vya korona. Juhudi zinafanywa na
mashirika mbalimbali ya afya duniani
ili kupata tiba.
Kila nchi ina mfumo wake wa kupambana
na Korona.
Mambo ya kujua kuhusu virusi vya
Korona;
- Kutembea juani,sehemu yenye joto au baridi au kuoga maji ya moto hakuzuii maambukizi,
- Maambukizi ya korona yanapona kama magonjwa mengine,kuna uwezekano wa kupata maambukizi mapya baada ya kupona,
- Kunywa pombe hakuzuii maambukizi,
- Kuvuta sigara kunachangia maendeleo ya mgonjwa kuwa mabaya,
- Mbu hawaambukizi korona,
- Kufunika uso kwa kitambaa hakuzuii maambukizi,
- Antibiyotik au dawa za malaria haziponyi korona ingawa kuna baadhi ya majaribio ya mchanganyiko wa dawa zinatomia dawa za malaria na virusi.
Maoni
Chapisha Maoni