Utangulizi Kichaa cha mbwa ni nini? Ni ugonjwa hatari unaotokana na maambukizi ya virusi vijulikanavyo kama rabies kwa kiingereza. Maambukizi hayo hutokea baada ya kung'atwa, kukwaruzwa na makucha au kulambwa machoni,puani, mdomoni au katika jeraha na mbwa, paka au popo aliye na virusi hivyo. Tofauti na virusi,unapong'atwa na mbwa au paka ni hatari ya kupata maambukizi ya bakteria katika majeraha ambayo husababisha maumivu makali na kuchelewesha kupona kwa majeraha hayo kama hatua hazitachukuliwa haraka. Lakini pia kupata majeraha sehemu za viungo( joints ) kunaweza kumsababishia mgonjwa ulemavu wa kudumu. Nchini Tanzania pekee inasadikiwa kuwa watu 1500 hufariki kila mwaka kutokana na kichaa cha mbwa, ugonjwa unaoweza kuzuiwa kwa asilimia 100 kwa kutumia chanjo(DW). Nini cha kufanya unaposhambuliwa na mbwa, paka au popo? Kuna hatua muhimu kadhaa za kufanya pindi unaposhambuliwa na mbwa, paka au popo. Safisha majeraha kwa maji yanayotiririka na sabuni bila kusugu...
Elimu ya Afya Kiganjani Mwako