Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Homa ya Findofindo (Tonsillitis)


Utangulizi 

Findofindo ( Tonsillitis) ni nini?

 Mafindofindo ni mashambulizi ya virusi au bakteria kwenye tezi za koo zijulikanazo kama findo. Asilimia 15 mpaka 30 ya mashambulizi haya yanatokana na bakteria ila asilimia kubwa hutokana na virusi. 



Dalili za mafindofindo 

Kwa kawaida ni ngumu kutofautisha kati ya maambukizi yatokanayo na bakteria na yale ya virusi ila leo nitakujuza siri ndogo. Zipo dalili za pamoja na zile za tofauti. 
Zifuatazo ni dalili za pamoja za mafindofindo unazoweza kuzipata kwa wagonjwa waliopata maambukizi ya bakteria na yale virusi 
  • Maumivu ya koo
  • Kupata shida katika kumeza 
  • Homa kali ( Zaidi ya nyuzi joto 38 za sentigredi) 
  • Maumivu ya kichwa
  •  Maumivu ya sikio 
  • Utando katika findo
Dalili zifuatazo zinaasilimia kubwa sana kupatikana kwa mtu mwenye mashambulio yatokanayo na virusi.
  •  Homa ( zaidi ya nyuzi joto 38 za sentigredi) 
  •  Uvimbe shingoni ( upande mmoja au pande mbili) 
  •  Maumivu ya kichwa 
  • Kutokwa na kamasi 
  • Kutokwa na machozi 
  •  Kumeza kwa shida 
  • Maumivu ya koo 
  • Utando mweupe koni 
  •  Kikohozi 
  •  Kupiga chafya

Je ni nini cha kufanya pindi unapokuwa na  dalili hizi? 

Pindi uonapo dalili hizi ni vizuri kufika kituo cha afya kwani kama maambukizi haya yanatokana na bakteria basi utalazimika kutumia dawa malum kwa ajili ya kuua bakteria ( Antibiotics) lakini kama maambukizi yanatokana na virusi basi hutohitajika kutumia dawa hizo na badala yake utashauriwa kutumia dawa za maumivu na kunywa maji mengi kwa siku. 

Ujumbe muhimu

Tambua tofauti za mashambulizi ya virusi na yale ya bakteria ili ukwepe kutumia antibiotics bila sababu.



                                                

                                                    Imetayarishwa na Dr. Umari Ali Jokho,MD.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Msongo wa Mawazo (Depression)

Msongo wa mawazo ni nini? Msongo wa mawazo  ( Depression ) ni mfadhaiko wa akili anaoupata mtu kutokana na shida, taabu, dhiki, matatizo au changamoto zinazomkabili katika maisha ya kila siku. Msongo wa mawazo hutokana na pale mtu anaposhindwa kukabiliana na jambo linalomtatiza. Msongo wa mawazo huwapata watu wa rika na asili zote. Tafiti zinaonyesha kuwa wanawake  hupata msongo wa  mawazo zaidi kuliko wanaume. Msongo wa mawazo ni tatizo la kimwili pamoja na kiakili. Dalili. kujisikia maumivu sehemu mbalimbali za mwili hasa kichwa, kukosa hamu ya kula au kula chakula kupitiliza,hasa vyakula vyenye madhara, kukosa hamu ya tendo la ndoa, kuwa na huzuni wakati wote na kujisikia mnyonge, kusahau kirahisi au kupungua kwa uwezo wa kufikiria, kujisikia mpweke au kukosa matumaini ya maisha, kupungua kwa uwezo wa kimasomo kwa wanafunzi, kuwa na hofu au kutokujiamini, kupungua au kuongezeka uzito bila kupenda, kushindwa kulala au kulala kupindukia, kukosa utulivu w...

Ualbino (Albinism)

 Ualbino ni nini? Ualbino ( albinism ) ni hali ya kiafya inayotokana na mwili kukosa uwezo wa kutoa homoni aina ya melanin . Homoni hii pamoja na kazi nyingine inahusika na utoaji wa rangi ya mwili. Ukosefu wa melanin huathiri ngozi, macho na nywele.  Ualbino ni hali ya kurithi kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Ikumbukwe kuwa  Albino sio mgonjwa bali ni mlemavu wa macho, nywele na ngozi ambavyo huathiri maisha yake ya kila siku, hata kufupisha umri wa kuishi. Nje na binadamu ualbino unaathiri pia wanyama, samaki, wadudu, nyoka, mijusi, ndege na hata mimea (kwa mimea hutokana na ukosefu wa klorofili).  Waathiriwa wenyewe nchini Tanzania waliamua kupendelea kuitwa "watu wenye ualbino" kutokana na matumizi mabaya ya neno zeruzeru katika utamaduni wa Afrika ya Mashariki ambako watu mara nyingi waliona uhusiano kati ya waathiriwa na mapepo au mizimu. Kuenea kwa Ualbino Tafiti zinaonyesha kuwa mtu mmoja kati ya 20,000 duniani ni albino, lakini kwa sababu zisizofahamika ba...