Kukua Kwa Tezi Dume ( Benign Prostatic Hyperplasia) ni nini? Ni ukuaji wa tezi dume ambalo lipo kwenye mfumo wa uzazi wa mwanaume hivyo kusababisha matatizo mengi hasa ya kibofu, figo na njia ya mkojo kwa ujumla. Hii hutokana na kuzibwa kwa njia ya mkojo kitu ambacho huleta madhara kwenye viungo husika. Tatizo hili huzidi kadri umri unavyoongezeka. Kwa kawaida ukubwa wa tezi ni sawa na kipira cha golf , lakini linaweza kukua hadi kufikia ukubwa wa chungwa hivyo kusababisha matatizo. Tezi dume kazi yake ni kutoa majimaji ya shahawa ( semen ) yanayosaidia kulinda, kurutubisha na kusafirisha mbegu za kiume ( sperms ) ndani ya mfumo wa uzazi wa mwanamke. Karibu nusu ya wanaume wenye umri kati ya miaka 51 mpaka 60 na zaidi ya asilimia 90 ya wenye umri wa miaka 80 na zaidi wana tatizo hili. Ukuaji wa tezi dume sio saratani lakini wakati mwingine vyote viwili humpata mtu mmoja. Dalili Kujisikia kukojoa muda wote au kushindwa kubana mjoko, Kukojoa kila mara ha...
Elimu ya Afya Kiganjani Mwako