Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers)


Ni vidonda vinavyotokea kwenye ukuta wa ndani wa tumbo au utumbo mwembamba.  Hutokana na tindikali(stomach acids) zinazotolewa na tumbo kusaidia mmeng'enyo wa chakula kuzidi hivyo kuharibu ukuta wa tumbo au utumbo mwembamba. 




Watu wengi wanaweza kuwa vidonda vya tumbo bila kuwa na dalili zozote. Lakini wakati mwingine vidonda vinaweza kutoka damu hadi kuhatarisha maisha kama hatua za dharura hazitachukuliwa.



Sababu

  • Sababu kubwa ya vidonda vya tumbo ni maambukizi ya bakteria anayefahamika kwa jina  la Helicobacter pylori(H. pylori). 
  • Matumizi ya dawa za maumivu kama vile ibuprofen(advil,ibucold, motrin IB n.k), aspirin, na naproxen  kwa muda mrefu.
  • Pombe na sigara.


Msongo wa mawazo na matumizi ya viungo vya chakula havisababishi vidonda vya tumbo lakini vinazidisha dalili za maumivu kwa mtu ambaye tayari ana vidonda.


Dalili




  • Maumivu ya tumbo sehemu iliyopo  kati ya kitovu na kifua, hasa wakati wa njaa kama vile usiku au kati ya mlo mmoja hadi mwingine. Maumivu hupungua baada ya kula au kutumia dawa za anti-asidi lakini baada ya muda huanza tena,
  • Kichefuchefu,
  • Kukosa hamu ya kula,
  • Kucheua mara kwa mara au kupatwa na kiungulia,
  • Kushindwa kula vyakula vya mafuta,
  • Kutapika damu au kupata choo chenye damu au rangi nyeusi,
  • Kujisikia unyonge au kuzimia,
  • Mwili kupungua uzito bila sababu.
Una hatari zaidi ya kupata vidonda vya tumbo kama una haya yafuatayo:
  • Una umri wa miaka 65 au zaidi,
  • Una maambukizi ya vimelea vya H. pylori,
  • Unatumia dawa za maumivu zaidi ya aina moja,
  • Ulishawahi kupata vidonda vya tumbo kabla,
  • Unatumia dawa za steroid.

Pindi utapata dalili mojawapo au kadhaa kati ya hizo hapo juu, daktari atakuuliza kama umetumia kwa muda mrefu dawa za maumivu. Majibu yako yanaweza kutosha kuanzisha matibabu ya anti-asidi na dawa za kupunguza utoaji wa tindikali (PPI). 

Daktari hulazimika kufanya vipimo vya ziada kama dalili zimezidi au mgonjwa ana hali mbaya. Vipimo hivyo ni kama vile pumzi, kupima haja kubwa kwa ajili ya vimelea vya H. pylori. Wakati mwingine kipimo cha kamera tumboni (Endoscopy) hutumika kwa ajili ya  kuchukua sampuli ili kuangalia kama kuna vimelea na kutambua pia ukubwa wa vidonda pamoja na kupambana na tatizo la kutokwa na damu.
 

Tiba

Ili kupunguza uwezekano wa kupata vidonda vya tumbo wakati unatumia dawa za maumivu;
  • Tumia dozi ndogo kabisa ili kudhibiti dalili na uache kuzitumia mara tu unapokuwa huzihitaji tena,
  • Tumia ukiwa umeshiba,
  • Usinywe pombe au kuvuta sigara wakati unatumia dawa za maumivu,
  • Tumia dawa za kupunguza tindikali kama vile Omeprazole, Pantoprazole n.k, pamoja na anti-acids,
  • Kunywa maji safi na salama,
  • Nawa mikono wakati wa kula,
  • Jifunze kupambana na msongo wa mawazo,
  • Punguza viungo vya chakula unapokuwa na maumivu ya tumbo.
Daktari atakuandikia antibiotics ili kupambana na vimelea vya H. pylori kama vitaonekana kwenye vipimo. Aina za antibiotics na dozi  zipo nje ya makala hii. 







 Ikumbukwe kuwa watu wawili kati ya watatu dunia wana maambuki ya H. pylori lakini wengi hawana vidonda vya tumbo. 




Maoni

  1. Entry-level woodworkers, hobbyists, and small business owners alike, select the Laguna Tools iQ Series desktop CNC routers when they are in search of a compact, space-saving CNC router. The benchtop CNC router is ideal for anyone in search of a user-friendly machine that doesn’t sacrifice quality for affordability. With a work envelope of 2′ x 3′ or 2′ x 4′, this machine can deal with a wide range|a variety} of prototyping and small manufacturing tasks. Laguna Tools® is a number one} and trusted brand of CNCs and industrial equipment for over forty years. Our machines are world-class and unequalled in terms of|in relation to} quality and precision. We supply a wide range|a Direct CNC variety} of products which might be} reliable, affordable, and cater to an increasing variety of industries.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Msongo wa Mawazo (Depression)

Msongo wa mawazo ni nini? Msongo wa mawazo  ( Depression ) ni mfadhaiko wa akili anaoupata mtu kutokana na shida, taabu, dhiki, matatizo au changamoto zinazomkabili katika maisha ya kila siku. Msongo wa mawazo hutokana na pale mtu anaposhindwa kukabiliana na jambo linalomtatiza. Msongo wa mawazo huwapata watu wa rika na asili zote. Tafiti zinaonyesha kuwa wanawake  hupata msongo wa  mawazo zaidi kuliko wanaume. Msongo wa mawazo ni tatizo la kimwili pamoja na kiakili. Dalili. kujisikia maumivu sehemu mbalimbali za mwili hasa kichwa, kukosa hamu ya kula au kula chakula kupitiliza,hasa vyakula vyenye madhara, kukosa hamu ya tendo la ndoa, kuwa na huzuni wakati wote na kujisikia mnyonge, kusahau kirahisi au kupungua kwa uwezo wa kufikiria, kujisikia mpweke au kukosa matumaini ya maisha, kupungua kwa uwezo wa kimasomo kwa wanafunzi, kuwa na hofu au kutokujiamini, kupungua au kuongezeka uzito bila kupenda, kushindwa kulala au kulala kupindukia, kukosa utulivu w...

Ualbino (Albinism)

 Ualbino ni nini? Ualbino ( albinism ) ni hali ya kiafya inayotokana na mwili kukosa uwezo wa kutoa homoni aina ya melanin . Homoni hii pamoja na kazi nyingine inahusika na utoaji wa rangi ya mwili. Ukosefu wa melanin huathiri ngozi, macho na nywele.  Ualbino ni hali ya kurithi kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Ikumbukwe kuwa  Albino sio mgonjwa bali ni mlemavu wa macho, nywele na ngozi ambavyo huathiri maisha yake ya kila siku, hata kufupisha umri wa kuishi. Nje na binadamu ualbino unaathiri pia wanyama, samaki, wadudu, nyoka, mijusi, ndege na hata mimea (kwa mimea hutokana na ukosefu wa klorofili).  Waathiriwa wenyewe nchini Tanzania waliamua kupendelea kuitwa "watu wenye ualbino" kutokana na matumizi mabaya ya neno zeruzeru katika utamaduni wa Afrika ya Mashariki ambako watu mara nyingi waliona uhusiano kati ya waathiriwa na mapepo au mizimu. Kuenea kwa Ualbino Tafiti zinaonyesha kuwa mtu mmoja kati ya 20,000 duniani ni albino, lakini kwa sababu zisizofahamika ba...

Homa ya Findofindo (Tonsillitis)

Utangulizi   Findofindo ( Tonsillitis) ni nini?  Mafindofindo ni mashambulizi ya virusi au bakteria kwenye tezi za koo zijulikanazo kama findo. Asilimia 15 mpaka 30 ya mashambulizi haya yanatokana na bakteria ila asilimia kubwa hutokana na virusi.  Dalili za mafindofindo   Kwa kawaida ni ngumu kutofautisha kati ya maambukizi yatokanayo na bakteria na yale ya virusi ila leo nitakujuza siri ndogo. Zipo dalili za pamoja na zile za tofauti.  Zifuatazo ni dalili za pamoja za mafindofindo unazoweza kuzipata kwa wagonjwa waliopata maambukizi ya bakteria na yale virusi  Maumivu ya koo Kupata shida katika kumeza  Homa kali ( Zaidi ya nyuzi joto 38 za sentigredi)  Maumivu ya kichwa  Maumivu ya sikio  Utando katika findo Dalili zifuatazo zinaasilimia kubwa sana kupatikana kwa mtu mwenye mashambulio yatokanayo na virusi.  Homa ( zaidi ya nyuzi joto 38 za sentigredi)   Uvimbe shingoni ( upande mmoja au pande mbili)   Maumivu...